WANANCHI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA KATIKA SIKU WADAU
Posted on: December 10th, 2023Wananchi mbalimbali katika Mkoa wa Morogoro na viunga vyake wajitokeza katika siku ya wadau iliyofanyika katika viwanja vya hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro mkabala na jengo la huduma za dharula(EMD) ambapo waliweza kupima afya zao.Huduma zilizotolewa ni magonjwa yanayotolewa upasuaji,magonjwa ya ndani,uchunguzi wa meno,masikio,pua na koo,saratani ya shingo ya kizazi na matiti,tezi dume kwa wanaume zaidi ya miaka 45,uzazi wa mpango,huduma ya maabara,huduma ya radiolojia na picha.